Posts

NENO LA LEO

Basi atukuzwe Mungu awezae kufanya mambo yote, makubwa ya ajabu tuyawazayo na pia tuyawazayo....Daniel.1-

neno la leo

Namshukuru Mungu kwa kuwa ayafanyayo ni makubwa maana nina uhakika hakuna hata mmoja awezaye kugusa hata chembe ya utukufu wake bali Jina lake litabaki kutukuzwa daima milele. Kwamaana  kwa neema niyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyo mpasa kunia; bali awe na nia kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu  kiasi cha imani yake. Rum.12:3.  Basi katika hayo maana Mungu hugawa karama na vipawa ambavyo yeye aliwapa watoto wake ili kusudi lake lipate kutimilika katika utukufu wake. Basi kwa mwanzo huu maaana Mungu anena nasi kwa nia yane lake nasi kama kusudio lake tuyafanye yale Mungu atuagizayo ili twa neema yake tupate kuichuchumilia taji ile aliyotuahi. Neema ya Bwana Yesu na iwe nanyi nyote Amina.